Advertisements
RSS

Kamati Ya Bunge Yakubali Kodi Zirekebishwe

21 Jun

Dodoma, Tanzania

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, imeafiki maeneo mengi ya kodi na tozo mbalimbali yaliyopendekezwa na Serikali yafanyiwe marekebisho.

Kamati hiyo pia imeeleza kutoridhishwa na Serikali katika kasi ya kushughulikia misamaha ya kodi naimesisisitiza umuhimu wa nidhamu ya matumizi ya Serikali na uwezo wa kuongeza mapato.

“Kamati inaishauri Serikali kuonesha dhamira ya kweli kufanikisha lengo hilo (la kuimarisha taratibu za kukusanya mapato pamoja na kupunguza misamaha ya kodi) na kutoa taarifa ya utekelezaji mbele ya Kamati Januari 2013,”amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Andrew Chenge.

Chenge alikuwa akiwasilisha taarifa ya Kamati yake kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/13 pamoja na tathimini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa 2012/13.

“Kamati inaendelea kushauri kwamba Serikali iachane na mtindo wa kuibua matumizi mapya yasiyo ya dharura ambayo hayakuidhinishwa na Bunge wakati wa utekelezaji wa
Bajeti.

“Mtindo huo unavuruga bajeti na kupunguza uwezo wa kutoa fedha za matumizi mengineyo (OC) na matumizi ya maendeleo kama ilivyokusudiwa. Kamati inasisitiza umuhimu wa Serikali kubana matumizi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima,” alisema Chenge.

Katika kodi, wakati Kamati ikiafiki mapendekezo mengi ya Serikali, lakini Chenge alisema wametaka iyaangalie baadhi ya maeneo ikiwemo kodi kwenye shughuli mbalimbali zikiwamo za waendesha pikipiki (bodaboda), mama lishe na vibajaji kwa kuwa vinawapatia vipato halali kwa maana ya kujiajiri wenyewe.

Kamati hiyo imependekeza viwanda vya nguo nchini vipewe misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye bidhaa za nguo na mavazi na imetaka kuendelea kwa
kiwango cha sasa cha ushuru wa bidhaa za matumizi za muda wa maongezi ya simu wa asilimia 10.

“Aidha, Kamati inapendekeza ianzishwe kodi mpya itakayolipwa kwa anayesajiliwa upya au kubadilishiwa sim card. Kamati inapendekeza tozo ya Sh  1,000 kwa kadi,” alieleza mbunge huyo wa Bariadi Magharibi (CCM).

Pia wameishauri Serikali kupiga marufuku usafirishaji wa ngozi ghafi nje ya nchi kama ilivyofanya nchi jirani ya Uganda na Ethiopia. Serikali imependekeza kutoza ushuru wa kuuza nje kwa bidhaa ya ngozi kwa kiwango cha asilimia 90.
 

“Kwa upande wa SDL (Tozo ya Kuendeleza Stadi), Kamati inashauri ipungue kutoka asilimia 6 hadi 4 na wigo wa walipaji upanuliwe kwa kuhusisha baadhi ya taasisi na wakala wa Serikali,” alisema Chenge.

Pendekezo la Kamati ni asilimia 2 ipelekwe VETA na asilimia 2 ipelekwe kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, pengo litakalojitokeza Serikali iangalie vyanzo vingine vya kuweza kuliziba.

Posted by MJ

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on June 21, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s