Advertisements
RSS

Benki ya Afrika Yajivunia Mafanikio Yake

17 Jul

Dar es Salaam

RASILIMALIWATU  iliyo bora imetajwa kama moja ya siri za mafanikio ya Benki ya Afrika Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Ammish owusu-Amoah ameyasema hayo wakati wa sherehe ya mwaka ya wafanyakazi wa benki hiyo iliyohusisha pia familia zao mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

“Tunatambua na kujali watu wetu, mafanikio ya benki yetu yamechangiwa sana na utendaji kazi bora wanaouonesha,” amesema  Amoah.

Amesema sherehe hizo zinahusisha wanafamilia kwa kuwa wana mchango mkubwa katika kuwaongezea ari na kuwapatia moyo wafanyakazi wa benki katika utendaji wao wa kila siku.

Sherehe hizo pia zilishuhudiwa na kutolewa tuzo kwa wafanyakazi mbalimbali baada ya kufanya vyema katika nafasi zao za kazi.

Mmoja wao ni Sophia Mwema ambaye alitangazwa kuwa mfanyakazi bora Idara ya Rasilimaliwatu na Utawala.

Mwingine aliyetambuliwa alikuwa, Masumbuko Humuli aliyekuwa mfanyakazi bora kutoka Idara ya Fedha na Uhasibu ambaye kwa upande wake alitoa mwito kwa wafanyakazi wenzake kushirikiana zaidi ili kuifanya benki hiyo kufanikiwa zaidi katika wakati huu wa ushindani.

Tangu ianzishwe hapa nchini mwaka 2007, imeshafanikiwa kufungua matawi kumi mkoani Dar es Salaam na sita nje ya mkoa huo yakiwepo ya Morogoro, Tunduma, Mwanza, Moshi, Mbeya na  Arusha.

Benki hii ni moja ya mtandao wa kibenki unaofanya kazi katika nchi 15 ambazo ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Ghana, Ivory Coast, Mali, Niger na Senegal.  Nyingine ni Burundi, Djibouti, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda. Pia ina tawi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 17, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: