Advertisements
RSS

Kampuni 7 zafungiwa zabuni‏ za Umma

07 Oct

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), imezifungia kushiriki zabuni za
umma, kampuni saba pamoja na wakurugenzi wake kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukiuka mikataba waliyoingia na taasisi nunuzi na vitendo vya udanganyifu.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga alisema jana kuwa katika kampuni hizo, sita zimefungiwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Oktoba 2, 2015 hadi Oktoba mosi 2017 kwa kukiuka masharti ya mikataba.

Aidha alisema kampuni moja imefungiwa kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia Oktoba 2, 2015 hadi
Oktoba mosi 2025 kwa kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi wakati wa michakato ya zabuni.

Alizitaja kampuni zilizofungiwa kuwa ni M/s Intersystem Holdings Company Ltd ya Dodoma, M/s
PEMA TECH Company Limited ya Dar es Salaam, M/s Nyakire Investment Limited ya Dar es Salaam, M/s Kosemwa Prospects Company Limited ya Dar es Salam, M/s Perntels Company Limited ya Dar es Salaam na M/s Car and General Trading Limited pia ya Dar es Salaam.

Pia aliitaja kampuni ambayo imefungiwa kwa miaka 10 kuwa ni M/s Gagaja Contractors Company
Limited ya Morogoro .

Aidha Balozi Lumbanga alisema PPRA ipo mbioni kuanza kutumia mfumo mpya wa manunuzi kwa
njia ya kielektroniki (e-procurement system) ambao utasaidia kukomesha watu ambao wamekuwa wakibadilisha majina ya kampuni.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on October 7, 2015 in Tanzania News

 

Tags: , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: