Advertisements
RSS

Tag Archives: Dr.William Mgimwa

Kutoka Bungeni: Sheria Kuwabana Wafanyabiashara Wanaotumia Dola Nchini

Kutoka Bungeni: Sheria Kuwabana Wafanyabiashara Wanaotumia Dola Nchini

SERIKALI  inapanga kuipitia upya Sheria ya Fedha ili kuwabana wafanyabiashara nchini wanaotumia zaidi dola kuliko Shilingi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa , Serikali itafanya hivyo kukabiliana na kushuka kwa thamani ya Shilingi.

Waziri Mgimwa ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Bakari (CCM) aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti matumizi holela ya dola nchini.

Katika swali lake Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya kushuka kwa Shilingi ya Tanzania ni matumizi makubwa ya dola kwa takribani kila kitu.

“Siku hizi kila kitu tunalipa kwa dola, uwanja wa ndege tiketi tunalipa kwa dola hata shuleni kwa dola, Serikali inadhibitije matumizi haya?

Akijibu swali hilo, Dk Mgimwa alisema kama Serikali katika kutatua tatizo hilo itazingatia zaidi kuangalia Sheria ya Fedha iliyopo inazungumza nini kuhusu matumizi makubwa ya dola nchini na iwapo ina upungufu katika hilo irekebishwe.

Alisema pia wataangalia sheria hiyo inazungumza nini kuhusu kumruhusu Mtanzania kuweka akiba ya dola badala ya Shilingi.

“Lakini pia kwa upande wa pili, Serikali tunayafahamu malalamiko mengi kuhusu matumizi ya dola na tumejipanga kuyashughulikia,” alisema.

Katika swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alitaka kujua Serikali inadhibitije biashara ya maduka ya kubadilisha fedha yasitumike kama mirija ya kusafirishia dola nje ya nchi kinyume cha sheria.

Lakini pia mbunge huyo aliitaka Serikali ibainishe mikakati yake itakayokwamua wafanyabiashara wa ndani na kudhibiti ununuzi wa bidhaa zinatengenezwa nchini, kununuliwa kutoka nje huku akitolea mfano vijiti vya kuchokonoa meno.

Akijibu swali hilo, Dk Mgimwa alisema zipo sheria na taratibu zinazotumika kuongoza maduka hayo namna ya kufanya kazi na hadi sasa vyombo vinavyotumika kudhibiti maduka hayo havijatoa taarifa yoyote ya kuonesha kuwa maduka hayo yamekuwa yakifanya biashara zake kinyume na taratibu zilizopo.

“Lakini bado hoja inabaki palepale kuwa maduka haya yanatuhumiwa kufanya kazi kinyume na taratibu, Serikali tanayachukua malalamiko yote na kuyafuatilia lengo likiwa ni kuhakikisha yanafanyakazi inavyotakiwa,” alisisitiza.

Soma Hapa Taarifa Zaidi ya Bajeti ya Tanzania

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on July 12, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , , ,

Taasisi za fedha Zikiongezeka kiwango cha riba kitapungua – Dk. William Mgimwa

DODOMA:

WAZIRI wa Fedha, Dk William Mgimwa amesema kiwango cha riba kinachotozwa na taasisi za fedha zikiwamo benki nchini, zitapungua pindi taasisi hizo zitakapoongezeka.

DK. William Mgimwa, MP

“Sisi Serikali tunatazamia wakopeshaji hawa waongezeke ili waweze kushindana na riba ishuke”, alisema Dk Mgimwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) aliyehoji kwamba wastani wa riba katika benki ni asilimia 33 hali isiyomsaidia mwananchi.

Waziri huyo alisema mkopeshaji yeyote anatoza riba kwa kuangalia gharama ya kupata fedha, uwezo wa mkopaji, hatari kwa wakopaji, usalama wa mkopo na faida.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka (CCM), aliyetaka kusikia kauli ya Serikali kuhusu riba kubwa wanayotozwa wananchi kutokana na fedha zao kuweka benki, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema viwango hivyo vya juu vinatokana na Sera yenyewe ya Taifa ya taasisi ndogo za fedha ambayo inasema riba itapangwa na asasi husika bila kuingiliwa na Serikali, Benki Kuu wala wafadhili.

Hiyo inatokana na asasi, zinafahamu gharama za uendeshaji, usalama wa mikopo na mbinu za biashara.

Hizo hujumuishwa kwa pamoja katika kufanya maamuzi wakati wa kupanga viwango vya riba. Alisema Serikali ipo katika hatua nzuri ya kuboresha masijala ya ardhi ili kurahisisha upatikanaji wa hati za viwanja/mashamba zitakazoweza kutumiwa na wakopaji kama dhamana na hivyo kupunguza riba inayotozwa.

“Mkakati mwingine ni pamoja na kuweka mfumo wa kusimamia taasisi zinazokopesha kwa kutumia fedha zao wenyewe. Benki Kuu inaandaa mfumo wa kuelimisha jamii juu ya mambo yanayohusu fedha na mikopo, hii itasaidia kuondoa hali ya wananchi kutozwa riba kubwa kwa kukosa tu uelewa wa masuala ya mikopo, riba na mikataba ya mikopo,” alisema Naibu Waziri huyo.

 
Leave a comment

Posted by on June 29, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , ,

Serikali ya Tanzania Yatangaza Bajeti ya mwaka 2012/2013

Dr. Mgimwa - Waziri Wa Fedha Tanzania akionyesha mkoba wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2012/13

Dr. Mgimwa – Waziri Wa Fedha Tanzania akionyesha mkoba wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2012/13

Dodoma, Tanzania:  SERIKALI imetangaza bajeti ya shilingi trilioni 15 kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo imelenga kudhibiti mfumuko wa bei kwa kutangaza kutoa vibali vya kuingiza chakula kutoka nje, na kuwabana matajiri kwa kuongeza kodi ya bidhaa zisizokuwa za lazima.

Akisoma bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma jana, Dk Mgimwa pia alitangaza kwamba Serikali imepanua wigo wa Kodi ya Mishahara (Paye) na sasa itawagusa wafanyakazi wenye kipato cha kuanzia Sh170,000 badala ya Sh135,000 ya awali.

Amesema, Serikali pia imerejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutenga Sh7 bilioni kwa ajili ya kuchukua vijana 5,000.

Dk Mgimwa amelieleza Bunge kuwa, Serikali imeongeza kodi za bidhaa mbalimbali, zikiwemo, bia, soda, sigara, juisi zinazoingizwa kutoka nje na kufuta msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa magari kwa wote waliokuwa wananufaika na msamaha huo.

Alifafanua kwamba kodi ya vinywaji baridi imepanda kutoka Sh69 kwa lita hadi Sh83 na mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, imeshuka kutoka Sh425 kwa lita hadi 145 kwa lita.

Wabunge wameelezwa kuwa, kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, imepanda kutoka Sh1,345 kwa lita hadi 1,614 kwa lita.

Dk Mgimwa amesema, kodi ya vinywaji vikali imepanda kutoka Sh1,993 kwa lita hadi Sh2,392 kwa lita, bia inayotengenezwa nchini kwa nafaka na ambayo haijaoteshwa, kodi yake imepanda kutoka Sh248 kwa lita hadi Sh310 kwa lita. Bia nyingine zote kodi imepanda kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita.

Kuhusu ushuru wa bidhaa za sigara, Dk Mgimwa alisema, sigara zote zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayozalishwa nchini, kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh6,820 hadi Sh 8,210 kwa sigara 1,000.

Alisema Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayopatikana nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh16,114 hadi Sh19,410 na sigara nyingine zenye sifa tofauti na makundi hayo, kodi imepanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa sigara 1,000.

Alisema tumbaku ambayo ipo tayari kutengenezwa sigara (cut filler) kodi yake imepanda kutoka Sh14,780 hadi Sh17,736 kwa bunda la sigara 1,000 wakati ushuru wa cigars unabaki kuwa asilimia 30.

Katika bajeti hiyo, Waziri Dk Mgimwa alisema muda wa maongezi (airtime) kwenye simu za mkononi umeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 12.

Alisema lengo la hatua hiyo ni kuoanisha ushuru wa bidhaa unaotozwa na huduma hiyo katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kwa kipindi hiki ambacho nchi zipo katika Soko la Pamoja.

Alisema hatua hizo za ongezeko la ushuru wa bidhaa kwa pamoja, zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh144,054.9 milioni.

Waziri huyo alipendekeza kufanyika marekebisho kwenye sheria husika za kodi ya matangazo ya Serikali yanayotoa msamaha wa kodi kwenye magari kwa walengwa mbalimbali ili kuweka ukomo wa umri wa miaka minane kwa magari hayo badala ya miaka 10.

Alisema magari yenye umri wa zaidi ya miaka minane yatatozwa ushuru wa bidhaa wa asilimia 20. Lengo la hatua hiyo ni kupunguza wimbi la uingizaji magari chakavu na kulinda mazingira.

Alitangaza pia marekebisho katika ushuru wa forodha, ikiwemo kufuta msamaha wa ushuru wa forodha katika vitu mbalimbali vikiwemo magari yenye ujazo wa CC 3000 huku pia ushuru wa forodha ukifutwa katika bidhaa nyingine nyingi muhimu.

Alisema katika kuhamasisha na kuchochea ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki, vifaa vinavyotumika katika ufugaji na kurina asali vimepewa msamaha wa ushuru wa forodha vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi na wafugaji wa nyuki.

Alisema msamaha wa ushuru wa forodha kwenye migahawa ya majeshi ya ulinzi utaendelea kutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Alisema kumefanyika marekebisho katika Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya mwaka 2004 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwa wazalishaji wa vyakula vinavyotengenezwa mahsusi kwa lishe ya watoto wenye utapiamlo na watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Alisema kuwa katika Bajeti hiyo, pia wametoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi zinazotumika katika kutengeneza vifaa vya kufanyia uchunguzi wa magonjwa (medical diognastic kits) kwa kuwa vifaa hivyo hutozwa asilimia sifuri vinapoagizwa kutoka nje ya nchi.

Katika marekebisho hayo, utatolewa msamaha kwenye mitambo (machinery) na vipuri vyake vinavyotumika kwenye uchimbaji wa madini lakini hautahusisha vipuri vya magari vitakavyoagizwa na makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini.

Katika bajeti hiyo, pia umetolewa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyuma vinavyowekwa kwenye kingo za barabara na lengo lake ni kutoa unafuu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Alisema ushuru wa forodha umepunguzwa kwa ving’amuzi kutoka asilimia 25 hadi asilimia sifuri ili kuwezesha mabadiliko katika teknolojia ya analogia na kwenda katika teknologia ya digitali.

Alisema katika Bajeti hiyo, pia ushuru wa ngano umeondolewa kuwa asilimia 0 badala ya asilimia 35.

Alisema Serikali pia imesamehe VAT katika mashine za kutolea stakabadhi (electronic fiscal devices), ili kupunguza bei yake na kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa nazo, kuhamasisha matumizi yake na hivyo, kuongeza mapato ya Serikali.

Katika eneo hilo, Serikali imeondoa VAT kwa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia, kusafirisha na kusambaza gesi asilia ili kuongeza matumizi ya nishati hiyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kwenye magari, majumbani na viwandani.

Wafanyabiashara ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 hawatalipa kodi kuanzia Julai Mosi, mwaka huu. Dk Mgimwa alisema mpango huo umefanywa kulinda mapato ya Serikali.

Kabla ya msamaha huo, wafanyabiashara hao ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 walikuwa wanalipa Sh35,000.

Marekebisho mengine ya kodi ya mapato ni kuwa wenye mapato kati ya Sh3 milioni –Sh7.5 milioni watalipa Sh100,000 badala ya Sh95,000.

Waziri Mgimwa alisema Bajeti hiyo imejielekeza katika Kukuza Pato la Taifa kwa asilimia 6.8 mwaka 2012 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.4 mwaka 2011.

Malengo mengine ni kuimarisha miundombinu ya uchumi, ikijumuisha umeme, barabara, reli na bandari, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongezeka kwa mapato ya ndani yatakayofikia uwiano na Pato la Taifa wa asilimia 18 kwa mwaka 2012/13 kulinganisha na mwelekeo wa asilimia 16.9 mwaka 2011/12.

Dk Mgimwa alitaja malengo mengine kuwa ni pamoja na kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei ili urudi kwenye viwango vya tarakimu moja na kuwa na kiwango tengemavu cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

Malengo mengine ni kukuza mikopo kwa sekta binafsi kwa kiwango cha asilimia 20 ya Pato la Taifa ifikapo mwishoni mwa Juni 2013, sambamba na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo na wa kati, kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji na kujenga uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi na kifedha pamoja na kushiriki kwa ufanisi katika ushirikiano kikanda na kimataifa.

Kuhusu matumizi ya maendeleo, Waziri Mgimwa alisema itazingatia vipaumbele vya miundombinu ya umeme – mkazo ukiwa upatikanaji wake kwa kuongeza uzalishaji, usafirishaji na usambazaji na jumla Sh498.9 bilioni zimetengwa.

 

 
Leave a comment

Posted by on June 15, 2012 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , , , , , , , ,

Baraza Jipya La Mawaziri Tanzania; May 2012.

Je Huu ni Mwanzo mpya? Baraza hili Litakidhi matakwa ya Watanzania? #MonFinance inawatakia kila la Kheri katika Majukumu haya mliyopewa.

  • Balaza Jipya Limeongeza Idadi ya Mawaziri  wawili na Naibu waziri mmoja. 
  • Wizara ya Nishati na Madini Imegawanyishwa na sasa kuwa na Manaibu wawili.
  •  Mawaziri Sita wa zamani Wameondolewa. 
  •  Sura mpya tatu za mawaziri na Kumi za manaibu waziri Zimeingia Baraza Jipya.

Na Hili ndilo Baraza jipya Lililotangazwa jioni ya jana Kutokea Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI
1.         OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2.         OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
Naibu Waziri:
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
3.         OFISI  YA WAZIRI MKUU
 MAWAZIRI:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
MANAIBU WAZIRI:
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
4.         WIZARA
 Wizara Ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri: Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Naibu: Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri:  Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Naibu: (Sijampata Jina Huyu)
Wizara Ya Ujenzi
Waziri: Dr.  John P. Magufuli, Mb.,
Naibu:  Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii
Waziri:  Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Naibu:  Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Wizara:  Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
 Naibu:  Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Wizara Ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Waziri:  Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Naibu:  Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Wizara Ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Waziri:  Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Naibu:  Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri: Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Naibu: Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
 Wizara Ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri: Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Naibu: Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Wizara Ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Waziri:  Dr. David M. David, Mb.,
 Naibu:  Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Wizara Ya Kazi na Ajira
Waziri:  Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Naibu:  Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Wizara Ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Waziri:  Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,
 Naibu:  Ndugu January Makamba, Mb.,
Wizara Ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Waziri: Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Naibu: Ndugu Goodluck J. Ole-Madeye, Mb.,
Wizara ya  Maji
Waziri:  Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Naibu:  Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
 Wizara Ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Waziri:  Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Naibu:  Ndugu Adam Malima, Mb.,
 
Wizara Ya Uchukuzi
Waziri:  Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Naibu:  Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Waziri: Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Naibu:  Ndugu Amos Makala, Mb.,
Wizara Ya Maliasili na Utalii
Waziri:  Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Naibu:  Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Wizara Ya Viwanda na Biashara
Waziri:  Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Naibu:  Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Wizara ya Fedha
Waziri:  Dr. William Mgimwa, Mb.,
Naibu:  Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu:  Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri:  Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
Naibu:   Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu:  Stephen Maselle, Mb.,
 
4 Comments

Posted by on May 5, 2012 in Tanzania News

 

Tags: , , , , , ,

 
%d bloggers like this: