RSS

Tag Archives: Monica Joseph

Salam zangu za siku ya Wanawake Duniani

Salam zangu za siku ya Wanawake Duniani

Ninawatakia wanawake wenzangu‎ Ulimwenguni kote, Heri ya Siku ya Mwakamke

a7caeb96fbdcd21385508290de4f359f“Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima”. ( Women should view their gender as a resource rather than a liability) – MJ

Ningependa kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni.

historia ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni wanaopitia changamoto mbalimbali.‎ Nililelewa katika mazingira kandamizi ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike…Kwa mfano kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa. Bibi yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi.

Kwa taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake, hatopitia shida alizopitia yeye…na hivyo siku zote alikuwa akiniasa kwamba “Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na mtoto wa Kiume”. Aliniimarisha kifikra na kiakili. Na siku zote alikuwa na msemo wake “Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi”- ushauri wake ndio ulikuwa dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza. Hadi hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika jamii…ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani. Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake.

Waswahili wana msemo usemao maisha ni shule…..msemo huu nimeuishi katika maisha yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia katika kampuni‎ ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu. Utekelezaji wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na wanaume.‎ Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu ‘hawala wa fulani’. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa mwanamke.

Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya aina hiyo. Kila nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya bibi ndio ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha – Monfinance Investment Group Ltd. Mbali na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania.

Kwa ujumla siku zote za maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA. Ni jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases).‎

Tunaposherehekea siku ya Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane, tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa  50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi.

‎‎Mimi nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu, Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume. Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na familia na sio Jinsia yangu.

Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote, wanaume na wanawake.‎

Happy Women’s Day 2016.

Monica Joseph

 

 
2 Comments

Posted by on March 8, 2016 in Articles, Business News

 

Tags: , , , , , ,

Benki ya Afrika (BOA BANK) Yawajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar Kutengeneza Mpango wa Kujenga na Kuboresha Biashara Zao.‏

Mkufunzi wa Warsha ya ilioandaliwa na Bank of Africa Erick Chrispin akitowa Mada wakati wa Warsha hiyo iliowajumuisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali Zanzibar katika Kuboresha na Kujenga Biashara katika kutengeneza Mpango wa Biashara iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
 Washirikib wa Warsha hiyo wakifuatilia kwa makini Mada zinazowesilishwa wakati wa Warshi hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa.
 Washiriki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia Mada zikiwasilishwa 
 Mtoa Mada Ndg Erick Chirispin akisisitiza jambo wakati wa kutoa Mada katika Warsha hiyo. Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar katika Kujenga na Kuboresha Biashara katika kutengeneza Mpango wa Biashara.  
 Washiriki wakiwa Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia Mada . 

 

Washiriki wakichanjia wakati wa warsha hiyo.
Mshiriki wa Warsha ya kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Biashara na Kujenga na Kuboresha Biashara akichangia wakati wa warsha hiyo.
Mtoa Mada Ndg. Erick Chrispin akionesha kitabu chenye mpango wa Biashara wakati wa warsha hiyo kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar na Wadau ilioandaliwa na Bank Of Africa katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

 

 

 

 

 

 

Washiriki wa Warsha ya Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara Zanzibar katika kuandaa Mpango wa Biashara wakiwa nje ya ukumbi wakibadilishana mawazo wakati wa mapunziko ya mchana.
                        Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzinews.com,
 
Leave a comment

Posted by on March 2, 2016 in Business News, Tanzania News

 

Tags: , , , ,

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA TANZANIA (TNBC)

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi muda mfupi kabla ya kufungua na kuendesha mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi muda mfupi kabla ya kufungua na kuendesha mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
Katibu Mtendaji wa Baraaa la Biashara la Tanzania (TNBC) Bw. Raymond Mbilinyi akiongelea juu ya  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
 Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Washiriki wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisoma muhtasari wa  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka akisoma hotuba kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete Kufungua  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015.
  Rais Kikwete akifungua rasmi  mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015.
  Rais Kikwete akifungua rasmi mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015.
 Rais Kikwete akiongoza mkutano wa nane wa Baraza la Biashara Tanzania (TNBC) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi 
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka,
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka,
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka,
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na secretariate ya TNBC  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka,
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na watumishi wa  TNBC  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2015. Wengine toka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahaya Mzee, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation Dkt. Reginald Mengi Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Karibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Florens Turuka,
PICHA ZOTE NA IKULU
 
Leave a comment

Posted by on September 2, 2015 in Business News

 

Tags: , , , , , ,

Kenya top in affordable financial services

 • Kenya has been ranked first in a survey by a US-based think tank that examined access to affordable financial services.
 • Tanzania and Indonesia were found to have the best regulatory environment of the 21 countries surveyed.
MOBILE MONEY IN TANZANIA

MOBILE MONEY IN TANZANIA

The country achieved the overall top score for its financial inclusion efforts in the 2015 Brookings Financial and Digital Inclusion Project Report which is published by the Brooking s Institution, largely due to the growth of its mobile money market.

21 Countries were ranked on four aspects of financial inclusion, including country commitment, mobile capacity, regulatory environment and the adoption of traditional and digital financial services. Of these categories, Kenya ranked first only in adoption.

Kenya earned 89 per cent overall, followed by South Africa (80 per cent), Brazil (78 per cent), Rwanda and Uganda (75 per cent each), and Chile, Colombia, and Turkey (74 percent each).

The use of mobile money transactions has been on the rise in Kenya since its inception. Data from the Kenya National Bureau of Statistics indicate that in 2014, mobile money subscriptions reached 26.0 million, representing a penetration rate of about 60 per cent of the total population.

Cash deposits made through mobile money agents reached Sh1,269 billion in 2014, up from Sh1,033 billion in 2013, while total transfers increased by 24.7 per cent to Sh2,372 billion up from Sh1,902 billion.

Kenya was cited for allowing both banks and non-bank institutions, including mobile operators, to offer financial services. In 2012, for example, M-Shwari was launched in Kenya as a partnership between the Commercial Bank of Africa and Safaricom to offer interest-bearing accounts and microloans, reaching an increasing number of unbanked people.

South Africa was ranked top for mobile capacity, defined by indicators like the extent of 3G mobile network coverage, ease of mobile payments, and the number of active mobile money services in each country. Kenya was ranked second, tied with Indonesia, Bangladesh, Colombia, Rwanda, and Afghanistan.

Tanzania and Indonesia were found to have the best regulatory environment of the 21 countries surveyed, according to the report.

Regulatory environment indicators included non-bank led mobile financial services, regulations governing e-money, the inter-operability of mobile money platforms, client identification (know-your-customer) processes, and cash-in/cash-out capability at agent locations.

Tanzania, Rwanda and Uganda were among seven countries ranked joint top for country commitment.

Mpesa, the first mobile cash transfer service in Kenya, was launched by Safaricom in 2007. Earlier this year, Equity Bank, the latest entrant in the mobile banking market, launched a special thin SIM card that allows the bank’s customers to access the lender’s mobile virtual network without parting ways with the existing telecom operators.

Other highlights of Kenya’s performance metrics include twelfth place for country commitment and third place for regulatory environment.

The country also had the highest rate of mobile money account ownership of the FDIP countries, as well as a regulatory environment that promotes entry of bank and non-bank providers in the market and diverse offerings such as mobile savings and credit products.

According to the World Bank Global index database which is sited in the report, South Africa, which was ranked second overall in the Brookings study, had 75 percent of adults with bank accounts and five percent with non-bank financial products, while in Kenya 55 per cent of people aged 15 and above have a bank account.

 
Leave a comment

Posted by on September 2, 2015 in Business News

 

Tags: , , , ,

Benki ya Covenant yapata faida bil. 1.4‏

BENKI ya Covenant imetangaza kupata faida kubwa katika kipindi cha utoaji
wa huduma inayofikia shilingi bilioni 1.4 hadi Juni mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa leo (Jumanne) wakati benki hiyo inasheherekea miaka mitatu ya utoaji wa huduma kwa wateja nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja amesema wakati anazungumza na wakurugenzi wa Bodi, wafanyakazi na waandishi wa habari kuwa, wamepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kutokana na aina ya huduma
wanazotoa.

Mwambenja amesema, mafanikio hayo ni zaidi na matarajioya Benki Kuu ambayo iliamini
benki hiyo itaanza kutengeneza faidi baada ya miaka mitatu.

Amesema kuanzia Juni mwaka jana hadi Juni mwaka huu, pato la benki limeongezeka kutoka shilingi milioni 951 hadi kufikia shilingi bilioni 2.9.

Faida imeongezeka kutoka shilingi milioni tano hadi shilingi bilioni 1.4. Amana ilikuwa Sh bilioni 10.2 na imefikia Sh bilioni 13.4.

“Fedha za wahisani zimeongezeka kufikia Sh bilioni 2.23 licha ya mtaji huo kutumika katika
uanzishaji wa benki na hasara ya Sh milioni 500 iliyopatikana katika mwaka wa kwanza wa huduma,” alisema Mwambenja.

Alisema mafanikio hayo yametokana na ubora wa huduma ambazo zimebuniwa na kuwa benki ya kwanza kutoa aina ya huduma za kipekee kwa kulenga Watanzania
ambao wako katika sekta zisizo rasmi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Balozi Salome Sijaona,
amempongeza Mkurugenzi na wafanyakazi wa benki hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii.

Amesema, bodi inatambua mchango wa wafanyakazi hao na kuendelea kuboresha masilahi
yao, huku akisisitiza kuwa benki itaendelea kulenga Watanzania wasio katika sekta rasmi.

 
Leave a comment

Posted by on September 1, 2015 in Uncategorized

 

Tags: , , , ,

New Skills and Development Levy (SDL) regulations

Minister of Finance TZ                                                          Tanzania Finance Minister : MS. Saada Mkuya Salum

Introduction:

Skills and Development Levy: is a levy collected by TRA under the Vocational Education Training Act and Income Tax Act.

SDL is charged based on the gross pay of all payments made by the employer to the employees employed by such employer in the particular time. It is important to understand that SDL is due and payable by an employer.

The gross emoluments is a sum of amount from salaries, wages, payments in lieu of leave, fees, commissions, bonuses, gratuity, any subsistence travelling , entertainment or other allowance received by employee in respect of employment or service rendered.

New SDL regulations
A new requirement has been introduced for employers to file a monthly tax return in respect of Skills and Development Levy. Failure to file such a return may result in late filing penalties.
Part XIII of the Tax Administration Act, 2015 (“Consequential Amendments”) includes amendments to various pieces of tax legislation, including Section 16(1) of the Vocational Education and Training Act, Cap 82), which now reads as follows: “Every employer shall file with the Commissioner on or before the seventh day of each month a return setting out the total gross monthly emoluments payable by the employer to employees in respect of the preceding month and the levy payable with respect thereto”.
Employers should make note of the new filing obligation, and immediately file a return for July 2015 (if not already filed). Use

ITX 219.01.E – SDL- Monthly Return

So is the   Employer’s obligation:

 • To calculate the amount of the levy and pay the amount to Commissioners account to the respective Tax Region in which such employer is registered.

 The SDL payments shall be made using form ITX 300.01.E – Employment Taxes Payment Credit Slip.

 • To prepare a MONTHLY RETURN and submit to the TRA office on or before the 7th day of the month following the month of payroll.
 • To prepare and remit half year certificate which tally with the monthly returns submitted during the period.

Who is liable for SDL?

Any employer who employs four or more employees shall pay SDL from gross emoluments.

The rate applicable for SDL is 5% of the total emoluments paid to all employees during the month.

The employee includes permanent employees, part time employees, secondary employees, casual laborers etc.

The SDL shall not be charged to:

(a) a Government department or a public institution which is wholly financed by the Government;

(b) Diplomatic Missions;

(c) the United Nations and its organizations;

(d) international and other foreign institutions dealing with aid or technical assistance;

(e) religious institutions whose employees are solely employed to-

(i) administer places of worship; or

(ii) give religious instructions or generally to administer religion;

(f) charitable organizations; or

(g) local government authority.”.

I Submit!

MJ

 
Leave a comment

Posted by on August 14, 2015 in Uncategorized

 

Tags: , , , , , , , , , , , ,

HELLO….. NIMERUDI

 EMAIL: monfinance@yahoo.com          Follow Me on twitter @MissNiyu


EMAIL: info@monfinance.com Follow Me on twitter @MissNiyu

Ni Muda Mrefu sasa tangu niandike katika Blog Yangu. Zaidi ya Mwaka.  Well, A lot has happened since June 2014.

Kwanza nimebadilisha Kazi Kutoka nilipokuwa na kwenda Kampuni nyingine (Reason, Career Growth) , Pili Nimefanikiwa kusajili Kampuni yangu ambayo inaitwa Monfinance Investment Group Limited; Unaweza kubonyeza Link hiyo na kuona nini tunafanya na Tunapatikana wapi. Tatu katika Passion yangu ya kuendeleza wanawake wenzangu, nikiwa na Mwenzangu Tumesajili Kampuni (Non Profit Organization)   Ambayo itasaidia na  kuhamasisha Biashara kujumuishwa kwa Biashara za wanawake kwenye Public and Private sector. Women Suppliers Development is for every Tanzanian Business Woman! Maelezo zaidi yatakuja kadri siku zinavyokwenda.

Pamoja na hayo yote Bado nilikuwa na wajibika katika familia .

Kuanzia Leo nitajitahidi angalau niwape post Tatu kwa week.

Main Focus: Business; Finance; Tanzania Economy and 2015 Elections. Yes Elections cannot be ignored

“Every election is determined by the people who show up.” ―By Larry J Sabato in Pendulum Swing 

I hope we will all show up and practice our constitutional right!

Be safe and Stay Blessed

 

MJ

 
1 Comment

Posted by on August 5, 2015 in Uncategorized

 

Tags: , ,

 
%d bloggers like this: