RSS

Benki ya Covenant yapata faida bil. 1.4‏

01 Sep

BENKI ya Covenant imetangaza kupata faida kubwa katika kipindi cha utoaji
wa huduma inayofikia shilingi bilioni 1.4 hadi Juni mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa leo (Jumanne) wakati benki hiyo inasheherekea miaka mitatu ya utoaji wa huduma kwa wateja nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja amesema wakati anazungumza na wakurugenzi wa Bodi, wafanyakazi na waandishi wa habari kuwa, wamepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kutokana na aina ya huduma
wanazotoa.

Mwambenja amesema, mafanikio hayo ni zaidi na matarajioya Benki Kuu ambayo iliamini
benki hiyo itaanza kutengeneza faidi baada ya miaka mitatu.

Amesema kuanzia Juni mwaka jana hadi Juni mwaka huu, pato la benki limeongezeka kutoka shilingi milioni 951 hadi kufikia shilingi bilioni 2.9.

Faida imeongezeka kutoka shilingi milioni tano hadi shilingi bilioni 1.4. Amana ilikuwa Sh bilioni 10.2 na imefikia Sh bilioni 13.4.

“Fedha za wahisani zimeongezeka kufikia Sh bilioni 2.23 licha ya mtaji huo kutumika katika
uanzishaji wa benki na hasara ya Sh milioni 500 iliyopatikana katika mwaka wa kwanza wa huduma,” alisema Mwambenja.

Alisema mafanikio hayo yametokana na ubora wa huduma ambazo zimebuniwa na kuwa benki ya kwanza kutoa aina ya huduma za kipekee kwa kulenga Watanzania
ambao wako katika sekta zisizo rasmi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Balozi Salome Sijaona,
amempongeza Mkurugenzi na wafanyakazi wa benki hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii.

Amesema, bodi inatambua mchango wa wafanyakazi hao na kuendelea kuboresha masilahi
yao, huku akisisitiza kuwa benki itaendelea kulenga Watanzania wasio katika sekta rasmi.

 
Leave a comment

Posted by on September 1, 2015 in Uncategorized

 

Tags: , , , ,

Leave a comment